Skip to main content

BASATA NA SHINDANO LA MISS UTALII


WADAU WAIPONGEZA BASATA KURATIBU MATUKIO YA SANAA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepongezwa na wadau wa Sanaa kwa juhudi zake katika kusimamia na kuratibu matukio mbalimbali ya Sanaa hapa nchini na kuyafanya kudumu.
Pongezi hizo zimetolewa wiki hii na wadau wa Sanaa wakati wakichangia mjadala uliohusu miaka mitano ya shindano la miss utalii na sanaa ya urembo nchini kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA uliopo Ilala, Sharif Shamba.

Akizungumza wakati akieleza historia za shindano hilo, Rais wa Miss Utalii, Gideon Chipungahelo alisema kuwa, BASATA imekuwa bega kwa bega na shindano hilo katika kuhakikisha miongozo na kanuni mbalimbali za kuendesha mashindano zinafuatwa na kusisitiza kuwa, hiyo ndiyo sababu ya shindano hilo kuweza kupata baadhi ya mafanikio ya ndani na nje ya nchi.

“Naishukuru Serikali na BASATA, kila mara wamekuwa wakitoa maelekezo na miongozo ambayo imelifanya shindano hili kufikia mafanikio haya ingawa kumekuwa na changamoto kadhaa hasa za kukosa wadhamini” alisistiza Chipungahelo.

Aliongeza kuwa, BASATA imekuwa mara kwa mara ikikutana na kamati ya miss utalii na kuipa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini na wadau wa sanaa ya urembo ambao wamekuwa wakitoa michango ya kuliboresha shindano hilo.

Awali wadau wa Jukwaa la Sanaa walipata wasanii wa kutoa maoni na ushauri kuhusu shindano la miss utalii ambapo walitoa changamoto kadhaa na kushauri jinsi ya kuzitatua na kulifanya shindano hilo lizidi kusonga mbele

“Shindano hili ni zuri na ni kiungo kizuri cha kukuza utalii kama waandaaji watalisimamia vizuri, ni vema kuwa na kamati maalum ya uendeshaji inayowajibika na wadhamini waone umuhimu wa kulifadhili shindano hili” alishauri Mzee Mwali Ibrahim ambaye ni mwandishi wa habari za uchumi wa gazeti la Majira.
Aliishauri kamati ya miss utalii kuliunganisha shindano hilo na maendeleo ya sekta ya sanaa nchini.
Rais wa Shindano la Miss Utalii, Gideon Chipungahelo (Katikati) akiongea na wadau wa Sanaa kuhusu miaka mitano ya shindano hilo kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya BASATA. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Miss Utalii Aboubakar Omar na Mkuu wa Kitengo cha Matukio wa BASATA, Omary Mayanga

Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo wa Miss Utalii, Vikas Gupta akielezea mipango mipya ya shindano la miss utalii kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii.Kulia kwake ni Bw. Aboubakar na Chipungahelo.

Mkurugenzi wa Matukio, BASATA, Omary Mayanga akitoa ufafanuz wa masuala mbalimbali yaliyojitokeza kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii.

Mzee Mwali Ibrahim ambaye ni mwandishi wa habari za uchumi na utalii wa Business Times akieleza umuhimu wa shindano la Miss Utalii

Wadau wa Sanaa wakifuatilia majadiliano kuhusu miaka mitano ya shindano la Miss Utalii. Kwa hisani ya mdau Jane John.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...