
Fundi sudi maarufu
kama Mzee Kipara amefariki Kigogo kwenye nyumba ambayo alikuwa
amepangishiwa na kundi la sanaa ambalo alikuwa anafanyia kazi la Kaole.
Kwa taarifa ambazo tumezipata sasa hivi kutoka kwa mtu ambaye yupo
nyumbani kwa mzee Kipara, kwa sasa wanauandaa mwili wake kwenda
kuupeleka Hospitali ya mwananyamala kuuhifadhi.
Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho, kwa taarifa zaidi
tutawaletea hapo baadae.Kwa hisani ya Full Shwangwe.
Comments