Meneja
wa kinwaji cha Serengeti Lager kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Bw.
Allan Chonjo anayeendesha gari pamoja na Kanji ambaye pia ni mfanyakazi
wa kampuni hiyo wakiongoza msafara wakati ulipopita mitaa mbalimbali ya
jiji la Dar es salaam leo, kuutambulisha muonekano mpya wa nembo ya bia
ya Serengeti Lager huku ikiwa na ubora na viwango vilevile.
Mkurugenzi
wa FULLSHANGWE Bw. John Bukuku akisalimiana na Kamalade Ali Choki
mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo na bendi yake ambaye ndiye anayetoa
burudani katika promosheni hiyo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa FULLSHANGWE akipiga stori na maafande wa kikosi cha usalama
barabarani wakati walipokutana katika shughuli za promosheni hiyo
kwenye makutano ya barabara za Shauri Moyo na Uhuru.
Mpiga
gitaa la bass wa Extra Bongo akipiga gitaa huku mnenguaji wa bendi hiyo
akicheza mbele yake wakati msafara huo ulipopita katika barabara ya
Uhuru leo.
Comments