Mbwana
Samata kushoto akiwa katika hekaheka za kuwania mpira katika moja ya
michezo ya ligi ya huko DRC Congo ambako timu yake ya TP Mazembe
inashiriki.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa
(ITC) kwa wachezaji Mbwana Samata na Patrick Ochan waliojiunga na timu
ya TP Mazembe wakitokea Simba.
TFF
ilipokea maombi ya uhamisho huo wa kimataifa Januari 10 mwaka huu
kutoka Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu la Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo (FECOFA) kwa niaba ya TP Mazembe.
Kwa
kupata ITC maana yake ni kuwa Samata na Ochan sasa wanaweza kuichezea
TP Mazembe kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo mechi zake
za mchujo zinaanza mwezi ujao.
Pia
TP Mazembe inatakiwa kulipa asilimia 5 ya mauzo ya Samata ikiwa ni
mchango maalumu (Solidarity Contribution) kwa timu alizopitia mchezaji
huyo kwani hajafikisha umri wa miaka 23. Timu zitakazopata mgao wa
asilimia hiyo 5 ni Kimbangulile FC na Mbagala Market ambayo siku hizi
inaitwa African Lyon.
Kwa
mujibu wa kanuni za uhamisho wa wachezaji za Shirikisho la Kimataifa la
Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA) fedha hizo zinatakiwa kulipwa ndani ya
siku 30 tangu ITC ilipotolewa kwa mchezaji husika.Inatoka kwa mdau Full Shwangwe.
Comments