Umoja
wa Mataifa umefanya mkutano wa dharura hapo Jumanne (tarehe 31 Julai)
juu ya kusonga mbele kwa waasi wa M23 kuelekea makao makuu ya mkoa huo,
Goma. Baraza la Usalama pia linajadiliana kutoa taarifa ya kuwaonya
waasi wanaosemekana kuungwa mkono na Rwanda.
Kwa mujibu wa wanadiplomasia
katika Umoja wa Mataifa, Mjumbe Maalum wa Umoja huo kwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, Roger Meece, aliwapa wajumbe 15 wanachama wa
Baraza la Usalama taarifa fupi inayoonya juu ya kitisho kipya kwa
serikali ya nchi hiyo yenye utajiri wa rasilimali.
"Vikosi vya serikali vinaishiwa
na silaha na wanaviacha vijiji mikononi mwa M23. Hii inazusha masuala
kuhusu uwezo wa jeshi la serikali, kwani jeshi hilo limepata madhara
makubwa sana." Alisema Meece kwa mujibu wa wanadiplomasia hao.
M23 waelekea Goma
Comments