Mhariri
wa BBC Idhaa ya Kiswahili,Ali Saleh (pili kulia) akizungumza wadau
mbalimbali walioweza kufika kwenye hafla fupi ya Uzinduzi kipindi cha
Dira ya Dunia kupitia Televishioni ya Star TV hapa nchini,ikiwa ni
muendelezo wa kutanua wigo wao kwa wasikilizaji.hafla hii inafanyika
hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Harbour View,jijini Dar
es Salaam.wengine pichani kutoka Kulia ni Mtangazaji Mahiri wa Dira ya
Dunia,Salim Kikeke,Hassan Mhelela na Meneja Mipango na Utafiti wa Sahara
Media Group,Nathan Rwehabura.
Meneja
Mipango na Utafiti wa Sahara Media Group,Nathan Rwehabura akizungumzia
ushirikiano wa Kampini yake na BBC Idhaa ya Kiswahili.
Mtangazaji
wa BBC Idhaa ya Kiswahili hapa nchini,Hassan Mhelela akizungumza
machache wakati wa Uzinduzi huo.Kulia ni Mhariri wa BBC Idhaa ya
Kiswahili,Ali Saleh.
Comments