Stori: Shakoor Jongo na Musa Mateja
KUNA madai kwamba ule ‘mkoko’ wa kifahari wa staa wa maigizo Bongo, Jacqueline Wolper aina ya BMW X6 lenye Namba za Usajili T574 BXF linatarajiwa kuingizwa sokoni wakati wowote na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya muda aliopewa nyota huyo kulipia deni lake la kukwepa ushuru wa shilingi milioni 70 kupita bila mwenyewe kusema chochote.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ‘mchuma’ huo ambao ‘umetaitiwa’ na Kampuni ya Udalali ya Majembe ya jijini Dar es Salaam kwenye yadi yao ya Mikocheni, umekuwa ukipata wateja kila kukicha ambao wanakwenda kuulizia siku ya mnada.
Chanzo kingine kilisema kuwa mbali na wateja kumiminika yadi ya Majembe, kumekuwa na usumbufu mwingi kwenye ofisi za TRA, Posta jijini Dar ambapo baadhi ya matajiri nao wamekuwa wakilifukuzia gari hilo kwa lengo la kulinunua.
Comments