KUFUATIA hali ya afya ya msanii nyota kwenye tasnia ya muziki wa Bongofleva Naseeb Abdul a.k.a Diamond kutetereka hali hiyo imechangia kushindwa kuchukua matukio ya ujio wa filamu iliyokuwa inatarajia kuanza kurekodiwa hivi karibuni.
Kwa mujibu wa mtayarishaji wa wa filamu hiyo ,Selles Mapunda amefunguka kwa kusema kuwa kuumwa kwa msanii huyo kumefanya kuhahirisha kuchukuwa picha kwa ajili ya ujio huo.
"Hali ya msanii huyo inaendelea vizuri na tunatarajia hali itazidi kuwa nzuri na atakapopona tutaanza rasmi uchukuaji wa picha hizo," alisema Mapunda.
Alisema kama ilivyokuwa kwenye filamu ya Crazy Tenant aliyoigiza msanii Peter Msechu Mapunda aliongeza kuwa ujio wa filamu hiyo ulikuwa unatabiriwa na 'Diamond' kuwa filamu hiyo ipewe jina la 'Nimpendenani' kutokana na ngoma yake msanii huyo iitwayo jina hilo kufanya vema .
Hata hivyo mwandaaji wa filamu hiyo kutoka amedodosa kuwa katika filamu hiyo Diamond ambaye ni mhusika mkuu ataigiza na muigizaji mmoja wapo kati ya Wema Sepetu au Jokate Mwigelo.
Comments