HOTUBA YA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR, MHE. BALOZI
SEIF ALI IDDI KATIKA UFUNGAJI WA MKUTANO WA NANE WA BARAZA LA NANE LA WAWAKILISHI, ZANZIBAR TAREHE 10 AGOSTI, 2012
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi, akisoma hutuba ya kufunga Kikao
cha Bajeti kwa mwaka 2012/2013 bada ya kupitisha
Bajeti za Wizara za Serekali ya Mapinduzi Zanzibar.
|
1.Mheshimiwa Spika,
awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uzima,
afya njema na kutujaalia amani na utulivu katika Taifa letu.
Naomba pia nikushukuru wewe
binafsi Mheshimiwa Spika, kwa busara zako za kuweza kuliendesha Baraza
lako Tukufu kwa umakini na mafanikio makubwa.
Pia nawashukuru na kuwapongeza Naibu Spika na Wenyeviti wote kwa namna wanavyokusaidia
Mheshimiwa Spika katika
kuliongoza Baraza hili. Vile vile, nawashukuru Wenyeviti na Wajumbe wa
Kamati mbali mbali za kudumu kwa kazi zao nzuri wanazozifanya katika
kufuatilia utekelezaji wa Taasisi mbali mbali za Serikali na
kufanikisha mkutano huu.
2. Mheshimiwa Spika, Mkutano
huu wa Nane wa Baraza la nane umekuwa wa kihistoria katika nchi yetu
kutokana na mashirikiano makubwa ya Viongozi na Wajumbe wa Baraza na
Watendaji wa Taasisi za Serikali. Nawashukuru wote na naomba tuendelee
na mashirikiano haya mazuri.
3. Mheshimiwa Spika, kwa namna
ya kipekee napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Rais wetu mpendwa Dkt.
Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi kwa uongozi wake wa busara, hekima na unaozingatia maslahi ya
wananchi. Ni dhahiri kuwa bidii za Rais Shein zinaendelea kuzaa matunda
ya maendeleo katika sekta za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
4. Mheshimiwa Spika, vile vile
niwapongeze Waheshimiwa Mawaziri kwa kuwasilisha bajeti zao vizuri na
kuweza kujibu hoja mbali mbali zilizojitokeza kwa umahiri na uelewa
mkubwa.
5. Mheshimiwa Spika, napenda
pia niwashukuru Waheshimiwa Wawakilishi wenzangu wa Baraza lako Tukufu
kwa kujadili, kudadisi na hatimae kupitisha bajeti za mapato na
matumizi ya Wizara zetu. Naelewa kwamba hoja zao mbali mbali
walizoziibua zilikuwa na mwelekeo mzuri na nia njema ya kuisaidia
Serikali yetu ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Comments