Rais Jakaya Kikwete, Marehemu Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Meles Zenawi,
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
asubuhi ya jana, Jumanne, Agosti 21, 2012, amepokea kwa mshtuko mkubwa,
masikitiko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Waziri Mkuu wa Ethiopia,
Mheshimiwa Meles Zenawi, kilichotokea jana usiku nje ya nchi ambako
alikuwa anatibiwa.
Kufuatia taarifa hizo, Mheshimiwa
Rais Kikwete, kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, Serikali yake na kwa
niaba yake mwenyewe amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Ethiopia,
Mheshimiwa Girma Wolde-Giorgis.
Katika rambirambi zake kwa
Mheshimiwa Wolde-Georgis, Rais Kikwete amesema: “Tanzania imepokea kwa
mshtuko mkubwa, masikitiko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha
Mheshimiwa Meles Zenawi kilichotokea jana usiku.”
Comments