Mshambuliaji
wa Taifa Stars,Mrisho Ngassa (8) akitafuta namna ya kuweza kumpita beki
wa timu ya Botswana, Zebras Oscar Neenga wakati wa mechi Kirafiki ya
Kimataifa iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Molopolole mjini Gaborone
Bostwana, timu hizo zilitoka Sare ya kufungana mabao 3-3.
Mshambuliaji
wa timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars", Mrisho Ngassa akijaribu
kutaka kumtoka beki wa timu ya taifa ya Botswana,Zebras Edwin Elerile
wakati wa mechi ya Kimataifa ya Kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja
Molepolole nje kitogo ya jijini la Gaborone.timu hizo zilitoka Sare ya
kufungana mabao 3-3.Mabeki wa timu ya taifa "taifa stars" wakimwangilia
mshambuliaji wa timu ya taifa ya Botswana akifunga bao la tatu wakati wa
mechi ya kirafiki iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Molepolole mjini
Gaborone.TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imelazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 na wenyeji Botswana mjini Gaborone katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Katika mchezo huo, mabao ya Stars yalifungwa na Mwinyi Kazimoto, Erasto Nyoni ambaye baadaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu na Mrisho Ngassa.
Stars inatarajiwa kurejea Dar es Salaam kesho baada ya mechi hiyo, na wachezaji wa timu hiyo kujiunga na klabu zao, kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
SOURCE: BIN ZUBEIRY
Comments