Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Freemaan Mbowe amesema
kamwe haongozi kundi au genge la wasaka vyeo na madaraka ndani ya chama
chake bali anaongoza kundi la watu wanaopenda mabadiliko.Kiongozi huyo
amesema binafsi hawezi kwa sasa kusema atagombea Urais au Ubunge kwa
sababu huu si muda wake hata kidogo.
Mbowe
amesema mwanachama yeyote makini wa Chadema kwa sasa ni muda wa
kuwaunganisha wanachama na watanzania kwa ujumla na wala si muda wa
kuwagawa kukimbilia madaraka. Kiongozi huyo amesema ndiyo maana
makamanda wote wakiongozwa na Dr Slaa wamejichimbia vijijini kwa kazi
moja tu ya kueneza vuguvugu la mabadiliko-M4C.
Chanzo: Tanzania Daima.
Comments