ZITTO ASEMA YUMO KIONGOZI WA JUU WA SERIKALI YA SASA,WENGINE NI WA AWAMU YA MKAPA, ATISHIA KUWAANIKA
Waziri Kuvuli wa Fedha Zitto Kabwe wa Kambi ya Upinzani,akiwakilisha bajeti mbadala ya kambi hiyo Bungeni Dodoma jana. Picha na Emmanuel Herman |
Waandishi Wetu
TUHUMA
kwamba baadhi ya vigogo Serikali wameficha mabilioni ya fedha nchini
Uswisi jana ziliibuka tena bungeni, huku Kambi ya Upinzani ikidai kwamba
inawafahamu wahusika wa ufisadi huo na kutishia kuwataja ikiwa Serikali
haitawataja.
Naibu Kiongozi wa Upinzani
Bungeni, Zitto Kabwe aliitaka Serikali kuwataja kwa majina viongozi na
wafanyabiashara wakubwa walioficha Sh315.5 bilioni nchini Uswisi,
akisema kwamba watu hao “wanafahamika”.
Juni mwaka huu, Benki Kuu ya
Uswisi ilitoa taarifa inayoonyesha kuwapo kwa kiasi cha Sh315.5 bilioni
zilizotoroshwa Tanzania na kufichwa nchini humo na vigogo ambao ni
wanasiasa pamoja na wafanyabiashara.
Akiwasilisha hotuba ya kambi
yake kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Fedha na Uchumi bungeni
jana, Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa wizara hiyo alisema mmoja wa
viongozi wa juu wa Tanzania na baadhi ya mawaziri wa Serikali za awamu
zilizopita ni miongoni mwa wamiliki wa fedha hizo.
“Kambi ya Upinzani bungeni
imepata taarifa kuwa mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa Tanzania na
baadhi ya mawaziri wa awamu zilizopita ni miongoni mwa fedha hizi,”
alisema Zitto.
Pia aliitaka Serikali kuliambia
taifa ni hatua gani itakazochukua kurejesha fedha hizo pia kuwataka
wamiliki wake na kama ikishindwa, wao watawataja.
Comments