Na: Mahmoud Ahmad Arusha
Serekali
imetishia kuwatimua wawekezaji wa kampuni ya madini ya Tanzanite one
iliyopo Mererani wilayani Simanjiro iwapo watashindwa kulipa deni la
zaidi ya dola za kimarekani milioni 2.2 zilizotokana na ukwepaji kodi .
Katibu
mkuu wizara ya nishati na madini Eliakim Maswi alitangaza msimamo wa
serikali wa kupitia upya mikataba ya makampuni ya madini hapa nchini
baada ya kugundulika kuwa yapo makampuni kadhaa yamekuwa yakiendesha
shughuli zake za madini bila kulipa ushuru wa serikali kinyume cha
sheria.
Akizungumza
na chama cha wanunuzi na wauzaji wa madini nchini TAMIDA,jijini Arusha
jana,Maswi alisema kuwa kampuni ya Tanzanite one imekuwa ikikwepa kulipa
kodi ya mrahaba wa madini tangu mwaka 2004 hadi 2008 na kufikia kiasi
cha shilingi bilioni 3.4 fedha za kitanzania.
Alisema
kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikitumia ujanja wa kukwepa kulipa mrabaha wa
mauzo pale inapokuta soko la madini nje ya nchi limeongezeka na kwamba
serikali kupitia kitengo cha ukaguzi wa madini iliweza kubaini ukwepaji
huo wa kodi na kuiamuru kampuni hiyo kulipa kiasi hicho cha fedha au
ifungashe virago.
‘’tulibaini
ukwepaji wa ulipaji kodi kwa kampuni ya Tanzanite one baada ya
kuanzisha kitengo maalumu za ukaguzi wa migodi hapa nchini na
tulipoifikia kampuni hiyo ndipo tulipobaini imekwepa kulipa kodi kiasi
hicho,na hivi sasa tunaanza kupitia upya ikataba ya makampuni ya
madini’’alisema Maswi
Aidha
alifafanua kuwa kampuni hiyo iligoma kulipa deni hilo ikidai ni kubwa
sana ,ndipo serikali ilipotaka kufanya ukaguzi upya ,kupitia wakaguzi
wake , lakini kampuni hiyo iligoma na kudai kuwa ipo tayari kulipa deni
hilo .
Aliongeza kuwa iwapo kampuni hiyo ingegoma kulipa deni hilo serikali ilikuwa tayari kuwatimua na kuwamilikisha wazawa mgodi huo.
Kwa
mujibu wa kamishina wa madini kanda ya kaskazini Benjamin Mchwampaka
alisema kuwa tayari kampuni hiyo imeshaanza kulipa deni hilo na kwamba
hadi sasa imeshatoa malipo ya dola 200,000 zaidi ya fedha za kitanzania
milioni 310,huku serikali ikiitaka kuhakikisha inamaliza kulipa deni
hilo hadi kufikia jamuari mwaka 2013.
Hata
hivyo katibu huyo aliitaka TAMIDA kuisaidia serikali kuyafichua
makampuni yanayokwepa kulipa ushuru wa madini wakiwemo baadhi ya
wafanyabiashara wakubwa ili wachukuliwe hatua na kusisitiza kuwa kwa
sasa serikali imeanza mkakati wa kupitia upya mikataba ya makampuni ya
madini hapa nchini.
Comments