Helikopta
tatu za Uganda zikiwa njiani kuelekea Somalia zimepotea katika ardhi ya
Kenya. Maafisa wa jeshi la Kenya wamesema leo kwamba helikopta nne
ziliondoka Uganda na moja ikatuwa mjini Garissa.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi
la Kenya Bogita Ongeri, helikopta hizo zilipotea karibu na eneo la mlima
Kenya, lakini rubani mmoja aliweza kuwasiliana nao, akiomba msaada.
Kwa mujibu wa msemaji huyo, mvua
na hali mbaya ya hewa zilihujumu juhudi za uokozi na Ongeri akaongeza
kwamba kundi la waokowaji limepelekwa sehemu hiyo ya ajali.
Hata hivyo alisema hawafahamu
kwa uhakika ni wapi hasa ajali hiyo ilitokea kwa sababu bado hali ya
hewa ni mbaya. Helikopta hizo aina ya Mi-24 zinauwezo wa kubeba hadi
abiria wanane.
Comments