Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Agosti 15 mwaka huu itapambana na
Botswana (Zebras) katika mchezo maalumu wa Kalenda ya FIFA
utakaofanyika jijini Gaborone.
Tayari
Kocha Kim Poulsen alishatangaza kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia
kambini Agosti 8 mwaka huu tayari kwa mechi hiyo ya kirafiki ya
kujipima nguvu.
Comments