KATIBU
mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamis
Suleiman Dadi (kulia) akimkabidhi fomu za kuwania nafasi ya uenyekiti wa
jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo Majura ambaye pia ni mdau mkubwa wa
michezo nchini.
Na: Dina Ismail
Bulembo
ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (MRFA) na
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
alichukua fomu hizo na kuzirejesha jana hiyohiyo.
Akizungumza
mara baada ya kuchukua fomu hizo, Bulembo alisema kwamba amelazimika
kuwania nafasi hiyo ili kuifanyia makubwa jumuiya hiyo kwani ni
mwanachama halali wa CCM na mwenye sifa hivyo anawajibu wa kuwania
nafasi yoyote inayomfaa kwa lengo la kuendeleza mikakati iliyopo ndani
ya jumuiya hiyo.
Hata
hivyo, Bulembo ambaye katika uchaguzi uliopita aligombea nafasi hiyo na
kushika nafasi ya pili nyuma ya Balozi Athuman Juma Mhina ambaye sasa
ni marehemu, alisema ataweka wazi mikakati yake pindi atakapopitishwa na
halmashauri kuu ya CCM.
Bulembo
anakuwa mgombea wa saba kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo ambapo
awali wanachama waliojitosa ni pamoja na John Edward Machemba, Said
Ramadhan Bwanamdogo, Salim Hamis Chikago, Jasson Samson Rweikiza, Alfred
Joseph Mwambeleko na Alphonce John Siwale.
Naye
Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Hamis Suleiman Dadi,alisema zoezi la
uchukuaji na urejeshaji fomu wa nafasi mbalimbali katika jumuiya hiyo
lililoanza Agosti 22 litafikia tamati Agosti 29 mwaka huu.
Alisema
mbali na nafasi ya uenyekiti, tayari baadhi wa wanachama wamejitokeza
kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongoizi katika jumuiya
hiyo kwa upande wa Bara na Visiwani.
Alizitaja
nafasi nyingine ni pamoja na Baraza Kuu la Wazazi Bara na Zanzibar,
Wajumbe wa Kamati Kuu Wazazi kwa upande wa Bana na Visiwani, Jumuiya ya
Wazazi kwenda Umoja wa Wanawake (UWT) na Jumuiya ya Wazazi kwenda Umoja
wa Vijana (CCM).
Comments