KIUNGO
wa kimataifa wa Cameroon na klabu ya Arsenal ya England, Alexander Song
amejiunga rasmi na klabu ya Barcelona ya Hispania.
Song
aliwasili katika mji wa Barcelona leo baada ya taratibu za uhamisho wake
kukamilika, ambapo klabu hiyo imelipa ada ya uhamisho ya pauni milioni
15.
Arsenal haikuwa na kipingamizi kuhusu kuhama kwa kiungo huyo, ambaye ameshafanyiwa vipimo vya afya yake na kufuzu.
Kocha Mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger amekubali kumuuza Song kwa kile anachoamini kuwa, kutoonyesha uwezo mkubwa msimu uliopita.
Hata
hivyo, kuna habari kuwa, uamuzi wa Song kuhama umetokana na kushindwa
kwake kuelewana na viongozi katika suala la kuboresha mkataba wake.
Song, ambaye alikuwa akilipwa mshahara wa pauni 55,000 kwa wiki, alikuwa amebakiza miaka mitatu kwenye mkataba wake na Arsenal.
Comments