Mkuu wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya EU,Catherine Ashton
AFP
Mkuu
wa sera za kimataifa katika umoja wa ulaya Catherine Ashton na waziri
wa mambo ya kigeni wa Afrika ya kusini Maite Nkoana-Mashabane walifanya
mazungumzo juu ya vikwazo vilivyowekwa dhidi ya nchi ya Iran na
Zimbabwe.
Mazungumzo
hayo yalikuwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano wa kilele wa Umoja wa
Ulaya uliopangwa kufanyikia mjini Brussels nchini Ubelgiji tarehe 18
mwezi ujao ambapo raisi Jacob Zuma anatarajiwa kuhudhuria.
Waziri Mashabane alisema kuwa kuhusiana na vikwazo vya mafuta kwa Iran wamekubaliana kumtuma mjumbe kutoka Afrika kusini mjini Brussels kujadili matokeo ya vikwazo vya EU kwa Iran,na nchi nyingine za ukanda wa kusini mwa Afrika.

Comments