Inatoka kwa Mdau
Kwa
kawaida, ili mtoto azaliwe, ni lazima mwanamke afanye tendo la ndoa
akiwa katika siku zake za kupata ujauzito ambapo mimba hutungwa. Baada
ya mimba kutungwa, mtoto hukaa tumboni kwa muda wa miezi tisa mbapo
hupitia hatua mbalimbali za mabadiliko hadi kuwa binadamu aliyekamilika.
Inapotokea
kuwa kitoto kimetoka tumboni kwa namna yoyote ile, kikiwa na umri wa
chini ya miezi mitano (wiki ishirini), tatizo hilo huitwa Miscarriage.
Katika
hali hii, kitoto kinakuwa hakijakamilika na hakiwezi kujitegemea
chenyewe kwa mahitaji muhimu kama kupumua, jambo ambalo husababisha
kifo.
NB: Mtoto akitoka akiwa ameshapita umri wa miezi mitano, tatizo hilo huitwa pre-mature birth (kuzaa njiti).
NINI HUSABABISHA MISCARRIAGE?
Zipo sababu nyingi zinazosababisha ujauzito uchoropoke.
- Matatizo ya Vinasaba (Genetic Factors)
Hitilafu
katika kromosomu (Chromosomal abnormalities) ambayo husababisha
vinasaba kuwa katika hali isiyo ya kawaida, inatajwa kuwa sababu kubwa
zaidi inayosababisha ujauzito uchoropoke ukiwa na umri wa chini ya wiki
13.
Matatizo
haya husababisha damu ya mama ishindwe kuendana nay a mtoto na
kusababisha reactions ambazo humdhuru mtoto na kumfanya ashindwe
kuhimili hali ya tumboni kwa mama. Hivyo ujauzito kuharibika.
2. Upungufu wa Homoni (Progesterone Deficiency)
Homoni
ya Progesterone hufanya kazi kubwa kuanzia mamba inapotungwa mpaka
mtoto anapozaliwa. Progesterone ndiyo huchochea uimara wa ukuta wa
placenta ambao mtoto hujishikiza. Upungufu wa homoni hii husababisha
ukuta wa mji wa mimba kushindwa kuhimili uzito wa mtoto, hali ambayo
husababisha ujauzito kuharibika na kutoka kabla ya muda wake.
3. Umri Mkubwa
Kwa
kawaida, mwanamke anapofikisha umri wa miaka 35 au zaidi, misuli
(sphincters) ya mji wake wa uzazi hulegea na kupungua nguvu za kuweza
kuhimili na kutunza kiumbe kinachokuwa ndani ya mji wa uzazi. Kulegea
kwa misuli hii husababisha mimba kuchoropoka kwa urahisi.
4. Magonjwa
Wanawake
wanaosumbuliwa na magonjwa kama kisukari, unene kupindukia (obesity),
Polycystic Ovary Syndrome, malaria kali, magonjwa ya zinaa na mengineyo
huwa katika hatari kubwa ya mimba zao kutoka.
5. Hitilafu Katika Kizazi
Baadhi
ya wanawake huwa na mfuko wa mimba (uterus) ambao muundo wake siyo wa
kawaida (T- Shaped Uterus). Wanawake wenye tatizo hili, huwa na hatari
kubwa ya mimba zao kuharibika kabla ya kutimiza umri wa miezi tisa.
6. Maambukizi ya bakteria au fangasi
Maambukizi
ya bakteria au fangasi husababisha misuli ya kizazi kushambuliwa na
kisha kupoteza uwezo wake wa kuhifadhi ujauzito, jambo ambalo
husababisha mimba kuchoropoka.
Sababu nyingine ni pamoja matumizi ya pombe kali, uvutaji sigara, matumizi ya dawa za kulevya, kemikali, matatizo ya kurithi n.k
DALILI ZA MIMBA KUCHOROPOKA (Symptoms of a miscarriage):
1. Kutokwa na damu sehemu za siri
Dalili
kubwa za miscarriage ni mama mjamzito kutokwa na damu (nzito au
nyepesi) sehemu za siri kwa vipindi au mfululizo. Damu hizi hutoka kama
zile zitokazo mwanamke anapokuwa kwenye siku zake na huambatana na
maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu.
2. Maumivu makali ya viungo
Dalili
nyingine za mimba inayotaka kuchoropoka ni maumivu makali ya mgongo,
kiuno, nyonga na tumbo chini ya kitovu. Maumivu haya huanza taratibu
lakini huongezeka kadiri muda unavyozidi kusonga mbele. Pia huambatana
na kutokwa na damu kama ilivyoelewa hapo juu.
3. Kutokwa na uchafu sehemu za siri
Dalili
nyingine kubwa ya Miscarriage ni mama mjamzito kuanza kutokwa na uchafu
wenye rangi sambamba na mabonge ya damu sehemu za siri.
ANGALIZO:
Dalili hizi pekee hazitoshi kuashiria kuwa tayari ujauzito umeharibika
ila mama mjamzito anapoona moja kati ya dalili hizi au zote,
anashauriwa kuwahi hospitali kuonana na daktari haraka iwezekanavyo.
Endapo
mama atachelewa, atakuwa anajisababishia matatizo zaidi kwani sumu za
kiumbe kilichoharibika huharibu mfuko wa uzazi na kusababisha matatizo
makubwa siku za mbeleni ikiwemo ugumba.
JE, KUFANYA MAPENZI UKIWA MJAMZITO KUNA MADHARA?
Swali:
Pole na kazi dokta, mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 22. Nimeolewa
na hivi sasa nina ujauzito wa miezi mitano. Tatizo linalotusumbua mimi
na mume wangu ni kuwa, tangu nipate ujauzito hamu ya kushiriki tendo la
ndoa imeongezeka sana lakini tunaogopa kufanya kwa sababu tuliwahi
kuambiwa kuwa tunaweza kumdhuru mtoto tumboni na ujauzito kutoka.
Tunaomba ufafanuzi wako daktari, je ni kweli kuna madhara
kufanyamapenzi ukiwa mjamzito?
Msomaji, Hanang, Manyara
Jibu:
Siyo kweli kwamba kufanya mapenzi ukiwa mjamzito kutasababisha mimba
kuharibika na kutoka. Jambo la kuzingatia ni kutotumia staili
zinazobana au kuumiza tumbo au kufanya mapenzi kwa muda mrefu. Tendo
la ndoa linalofanywa kwa wastani husaidia kulainisha njia ya uzazi
hivyo kupunguza matatizo wakati wa kujifungua. Inashauriwa kuwa
ujauzito ukifikisha miezi nane, wanandoa waache kufanya tendo hilo
mpaka mama atakapojifungua na kupona.
KUZUIA MIMBA KUCHOROPOKA
Hakuna
tiba ya moja kwa moja inayoweza kuzuia tatizo la mamba kuchoropoka ila
kwa kuzingatia vyanzo vya tatizo hili, ni rahisi kuliepuka.
- kuacha tabia hatarishi
Tabia
kama ulevi wa kupindukia, matumizi ya dawa za kulevya na sigara kwa
wanawake wajawazito yakiepukwa, hupunguza hatari ya miscarriage.
- Kufanya mazoezi
Inashauriwa
kuwa, mama mjamzito ajenga mazoea ya kufanya mazoezi mepesi angalau
mara tatu kwa wiki kwa muda usiopungua nusu saa. Mazoezi kama kutembea
na mengine mepesi husaidia kuimarisha misuli ya kizazi na hivyo
kupunguza hatari ya mamba kuchoropoka.
- Vyakula
Inashauriwa
mama mjamzito kula vyakula vyenye madini ya Zinc, Magnesium, Vitamin B6
na Vitamin C kwa wingi ili kulinda ujauzito wake. Vyakula vitokanavyo
na nafaka, mimea jamii ya mikunde, karanga, kiini cha yai, mboga za
majani na matunda husaidia kuimarisha afya ya mama na mtoto hivyo
kuzuia tatizo hili.
- Kupata chanjo
Akina
mama wajawazito wanashauriwa kuhudhuria kliniki mara kwa mara kwa ajili
ya kupatiwa chanjo za magonjwa hatarishi ambayo husababisha ujauzito
kuharibika na kutoka.
- Kupima afya mara kwa mara
Akina
mama wajawazito ni lazima wajenge mazoea ya kwenda kupima afya zao mara
kwa mara na kuangalia uwepo wa magonjwa kama ya zinaa na mwengineyo, na
kama yapo watibiwe haraka ili kulinda kiumbe kilichopo tumboni.
Comments