Erick Evarist na Musa Mateja
SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwa amenasa kibendi, mwigizaji anayewakilisha Kundi la Scorpion Girls, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, amemtaja mwanaume anayeitwa Bushoke kwamba ndiye baba wa kijacho wake, Amani lina kila kitu.
Jini Kabula aliyaongea hayo mwanzoni mwa wiki hii, jijini Dar es Salaam baada ya kubanwa na mapaparazi wetu kufautia madai kwamba, mwanaume aliyempachika mimba ni mfanyabiashara wa madini.
Hata hivyo, staa huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema ‘anampeleleza’ Bushoke kama kweli ana nia na mtoto atakayezaliwa au maneno maneno tu.
Comments