Waziri wa zamani wa Serikali ya Muungano, Hassan Nassor Moyo
Na Mwinyi Sadallah
Baraza la Wazee wa CCM na UVCCM,
wameitaka jamii kuyatahadhari matamshi yanayotolewa na Waziri wa zamani
wa Serikali ya Muungano, Hassan Nassor Moyo, kuhusu mwelekeo na hatma ya
Tanzania.
Wakizungumza na NIPASHE kwa
nyakati tofauti, Wazee na UVCCM walimtaka Mzee Moyo kuyatafakari maoni
yaliotolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Julius
Nyerere, Profesa Issa Shivji.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa
CCM Zanzibar (BWCZ), Makame Mzee Suleiman, alisema matamshi ya Shivji
yana msingi ili kulilinda Taifa lisibomoke kinyume na mtazamo wa Moyo.
Akiyazungumzia matamshi ya Mzee
Moyo alidai yanaweza kutafsiriwa na wana jamii kama yanayotaka
kulisambaratisha Taifa ambalo limejengeka kwa misingi ya umoja wa
kitaifa.
Mwenyekiti huyo wa Wazee
Zanzibar, alisema hatakiwi kuyakebehi mawazo ya waasisi wa Muungano ila
kuuheshimu uoni wa kitaalam wa Shivj kwa utulivu na historia.
“Mzee mwenzangu hapaswi kuponda
mawazo ya waasisi wetu, ana wajinu na ulazima wa kuyatafakari kwa kina
maoni ya Shivji kuhusu hatma ya Muungano wa Serikali mbili,” alisema.
Comments