LAGOS, Nigeria
MCHEZA filamu mpya wa kike wa Nigeria, Ruth Bessong ameanza kuwatisha wakongwe wa fani hiyo, Genevieve Nnaji, Ini Edo na Mercy Johnson.
Ruth ameanza kuwatisha wakongwe hao kutokana na uwezo aliouonyesha katika filamu za Kinigeria alizozicheza hivi karibuni.
Mbali na kuonyesha uwezo wa hali ya juu kiuigizaji, Ruth pia amekuwa kivutio kikubwa kutokana na mwonekano wake wenye mvuto.
Mwanadada huyo, ambaye ni mzaliwa wa Jimbo la Cross-Rivers, ameelezewa kuwa ana kipaji cha aina yake katika fani hiyo na uelewa mpana kuhusu mambo mbalimbali.
Ruth, ambaye amesomea fani ya uigizaji kwenye chuo cha Royal Art Academy, ametabiriwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye fani hiyo nchini Nigeria, ambayo ni maarufu zaidi kwa jina la Nollywood.
Baadhi ya filamu, ambazo Ruth amecheza hadi sasa ni pamoja na ‘90 ninth Day’ iliyotayarishwa na Papel Images na tamthilia ya ‘Cross Roads,’ iliyotayarishwa na Emeka Ossai.
Ruth amewataja wacheza filamu wanaomvutia nchini Nigeria kuwa ni Genevieve, Ini na Mercy na kwa upande wa waigizaji wa Kihindi, alimtaja Alec Baldwin.
Kwa sasa, Ruth ni mwanafunzi katika chuo cha Houdegbe North American kilichopo mjini Cotonou, akisomea uhusiano wa kimataifa.
Mbali na uigizaji, Ruth anapenda kusoma, kuandika na kucheza na watoto.Inatoka kwa mdau.

Comments