Wananfunzi
wa Shule ya Msingi Mbezi ya Jijini Dar es Salaam, nao hawakuwa nyuma
katika kudai haki yao ambapo nao walifikisha ujumbe kwa njia hii ya
Bango, wakiwa pembezoni mwa barabara Morogoro Jumatatu ya tarehe
30.8.2012 asubuhi.
---
Hivi
majuzi nilishtushwa sana baada ya kusikia kuwa nao walimu wameamua
kufanya migomo ili kuitaka serikali iwalipe madai yao, niliogopa sana
na kuanza kujiuliza ni kitu gani kimetokea mpaka nchi yetu ya Tanzania
sasa imekuwa ni ya maandamano na migomo ya kila kukicha???.
Hali kadharika nilizidi kupata
mshangao pale niliona wanafunzi wa shule za msingi nao wameamua kufanya
maandamano kuwapinga walimu wao ambao waliamua kufanya mgomo ili
kuishinikiza serikali iwalipe madai yao.
Jambo la kujiuliza mwanamchi
mwenzangu ni nani aliyewapa ujasiri watoto hawa mpaka wakaandika
mabango na kuamua kuandamana??? Ni vyema wazazi pamoja serikali wakawa
macho kwa vile Taifa lisilo na misingi si taifa jema??? Tunapoelekea
kwa sasa umefika wakati viongozi kuacha kufumbia macho madai ya watu.
Sishangai kuona vijana hawa
wakiwa wakubwa wakafika hatua ya chuo kikuu kuendelea na migomo; ni
vyema tukaanza kukunja makucha yao ingali bado wadogo ili baadae wasije
kuleta madhara makubwa katika jamii maana wahenga walisema, "Samaki
Mkunje Angali Mbichi".
Pia ningewaomba wazazi kuacha
kufumbia macho haya ambayo yanatokea sasa maana hali hii ni hatari sana
katika familia na taifa letu kwa ujumla.
Comments