Johannesburg, Afrika Kusini
Lile shindano lililowabamba watu kibao ndani na
nje ya Bara la Afrika la Big Brother Africa ‘Stargame’, Jumapili iliyopita
lilifikia tamati ambapo mshiriki kutoka Sauzi, Keagan Petersen aliibuka kidedea
na kunyakua kitita cha dola 300,000 (zaidi ya Sh. Milioni 450) huku Prezoo
kutoka Kenya akishika nafasi ya pili.
Kwa mujibu wa wadau waliokuwa wanalifuatilia
shindano hilo, Prezoo aliyekuwa na nafasi kubwa ya kuibuka kidedea, ameponzwa
na tabia yake ya kucheza na mioyo ya mabinti mjengoni, kutokuwa mkweli kwenye
mapenzi kama ilivyotokea kwa Goldie na kupenda ugomvi na ulevi wa kupindukia,
mambo yaliyompunguzia mashabiki na hivyo kukosa kura nyingi.
Hata hivyo, licha ya kushika nafasi ya pili,
Prezoo amelamba dili la nguvu la kuwa balozi wa Kampeni ya ONE na kupata zali
la kwenda kuhudhuria shoo ya Jay Z nchini Marekani siku chache zijazo.
Washiriki kutoka Tanzania, Hilda na Julio
walitolewa katika hatua ya kwanza ya mtoano na kusababisha Watanzania wengi
wasiendelee kufuatilia shindano hilo.
Comments