Katibu
Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akimkabidhi kadi ya CHADEMA
aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kododo jimbo la
Mvomero, bwana Charles Kiwaga. Wengine ni wanachama wapya wa CHADEMA
tawi la Kododo Mvomero.
Aliyekuwa
Katibu Mwenezi wa CCM kata ya Muhonda akieleza jinsi alivyokunwa na
sera za CHADEMA zilizoelezwa na katibu Mkuu wa BAVICHA katika mkutano wa
hadhara katika kijiji cha Kichangani.
Mwenyekiti
wa serikali ya kitongoji cha Kododo, Charles Kiwaga (kulia) akifafanua
kero ya shule ya msingi kododo kwa kayibu mkuu wa Bavicha Deogratias
Munishi. Katikati ni mjumbe wa kamati ya maendeleo ya elimu ya shule
hiyo. Shule hii ina wanafunzi 652 na mwalimu mmoja tu.
Na Mdau Hellen-Morogoro
Operesheni
Sangara inayoendelea kwa upande wa Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la
CHADEMA (BAVICHA), Bwana Deogratias Munishi amezidi naye kupasua vijiji
ndani ya Mvomero, Morogoro. Pia wanavijiji walimuonyesha hali halisi ya
maendeleo katika kata yao ya Luale kwa kipindi kirefu walichokuwa chini
ya CCM tangu miaka 50 iliyopita mpaka sasa na wakiwa wamekata shauri
kujiunga na CHADEMA kama chachu ya mabadiliko. Inatoka kwa Mjengwa.
Comments