WADAU wengi wa tasnia ya filamu bongo wameanza kuingiwa na shaka kubwa, baada ya msanii wa filamu Christine John ‘Sintah’, kutumia jina la msanii wa Marekani Jennifer Lopez aka JLO, kwenye filamu yake na kazi hiyo inakwenda kwa jina la ‘The Return Of JLO’.
Mtandao mmoja , ulifanya mazungumzo na wadau kadhaa wa tasnia hiyo na wote walionekana kuwa na mawazo tofauti kuwa wanshindwa kuelewa ni kitu gani kilimfanya hadi mwanadada huyo kutumia jina mtu bila idhini yake.
Mwandishi alimtafuta ‘Sintah’, ili aweze kuwajibu wadau hao, katika kujibu kwake alidai kuwa ameamua kutumia jina hilo kwani huo ndiyo wakati wake yenye kwani anakuja kwa kishindo kikubwa katika tasnia cha filamu hivyo mashabiki wake waondoe shaka juu ya hilo.
Hata hivyo aliongeza kuwa sababu kutumia jina hilo kingine ni kwamba anampenda sana mwanadada huyo na haoni kama inaweza kuleta matatizo ingawa ni kweli hakuzugumza naye juu ya hilo.
“Ni kweli kwa msanii mwigine anaweza kunishtaki kwani nimetumia jina lake pasipo mwenyewe kujua, lakini nachowaomba watanzania wajue kila kitu kipo sawa na kazi yangu imetulia hivyo waitazame kwa umakini ili wajue kitu gani kinachozungumzwa,” alisema.
Comments