Hadi mapumziko, Simba inayotumia wachezaji wake wa kikosi cha pili, Simba B, kinachofundishwa na Suleiman Matola, walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na Rashid Ismail aliyeunganisha krosi ya Edward Christopher dakika ya pili tu ya mchezo huo.
Kipindi cha pili ‘Watoto wa Matola’ walirudi na moto na kulisakama kama nyuki lango la Azam, wakigongeana pasi za uhakika ndefu na fupi na kuwafunika kabisa mabingwa wa Kombe la Mapinduzi.
Christopher Edward aliifungia Simba bao la pili kwa penalti dakika ya 56, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa ndani ya eneo la hatari na Luckson Kakolaki.
Azam walipata bao la kufutia machozi dakika ya 71, mfungaji akiwa Zahor Pazi aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Gaudence Mwaikimba, baada ya kutokea purukushani kwenye lango la Simba B.
Ushindi huu wa Simba B ni sawa na kuwalipia kisasi kaka zao, Simba A ambao walifungwa na Azam 3-1 katika robo fainali ya Kombe la Kagame mwezi uliopita.
Simba; Abuu Hashimu(18), Miraj Adam (19), Omary Salum (11)/William Lucian ‘Gallas’, Hassan Isihaka (5), Hassan Hatibu (15) Said Ndemla (13), Haroun Athumani (7), Abdallah Seseme (17), Rashid Ismail (8), Edward Christopher (9)/Ramadhan Mzee na Frank Sekule (4)Ibrahim Ajibu.
Benchi; Saleh Malande (1), Ramadhan Mzee (2), William Lucian ‘Gallas’(3), Kenny Alex (12), Mohamed Salum (16), Ibrahim Ajibu (20) na Jesse Nyambo (14).
Kocha; Suleiman Matola. Msaidizi; Amri Said.'
Azam FC; Wandwi Jackson (18), Ibrahim Shikanda (21), Samir Hajji Nuhu (11), Said Mourad (15), Luckson Kakolaki (5), Abdulhalim Humud (24), Sunday Frank (12), Jabir Aziz (25)/Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba (17)/Zahor Pazi, Abdi Kassim (20) na Kipre Herman Tcheche (27)Hamisi Mcha.
Benchi; Aishi Mfula (1), Omary Mtaki (2), Himid Mao (23), Khamis Mcha (22), Kelvin Friday (28). Abdulghani Gullam (14) na Zahor Pazi (9).
Kocha; Boris Bunjak (Serbia). Msaidizi; Vivek Nagul (India).
Katika mchezo wa kwanza, Mtibwa Sugar ilitinga fainali kwa kishindo kwa kuinyuka Jamhuri ya Pemba mabao 5-1, ambayo yalitiwa kimiani na Babu Ally Seif dakika ya 15, Salvartoy Ntebe dakika ya 17, Mfaume Shaaban aliyejifunga dakika ya 38, Vincent Barnabas dakika ya 43 na Awadh Juma dakika ya 85 wakati la kufutia machozi la Jamhuri lilifungwa na Mbarouk Chande dakika ya 62.
SOURCE. BIN ZUBEIRY
Comments