Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Ofisi za Tawi la CCM Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja jana. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mjini Magharib, Mohammed Yussuf, wakati alipofika mkoa huo kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Ofisi za Tawi la CCM Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja jana. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) na mmoja kati ya wazee wa eneo hilo ambaye ni kati ya wazee waliokuwa na kucheza ‘Chandim’ pamoja. Hapa ilikuwa ni baada ya kuweka...