MWENYEKITI wa UVCCM, Mkoa wa
Arusha,kwa miaka mitano, James Ole Millya,ametangaza kujiuzulu nafasi
zote kuanzia Taifa hadi Mkoa na kutangaza kujiunga na Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa madai kuwa CCM imefilisika
kimawazo na haitoi matumaini kwa watanzania.
Aidha
alisema hawezi kuendelea kupanda gari lenye pancha lukuki, hivyo
ameamua kupanda gari lisilo na pancha na lenye kutoa matumaini mapya
kwa watanzania.
Hayo ameyasema leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Kibo Palace, iliyopo Jijini hapa.
Amesema mara nyingi alikuwa
akikemea mambo ambayo yanaweza kubomoa chama cha CCM kwa upendo, lakini
alikuwa akipuuzwa kwa sababu ya chama hicho kuwa na kikundi cha wenyewe.
“Mimi nanukuu maneneo ya
Nyerere kuwa alishawahi kusema CCM sio mama yangu na mimi pia CCM sio
mama yangu na natangaza rasmi, kuondoka ndani ya chama hiki na najiunga
na Chadema, sababu ndicho chama chenye kuleta tumaini jipya kwa
watanzania,”alisema.
Ametaja nafasi alizoachia ngazi
ni pamoja na Mjumbe kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa, Mjumbe kamati ya
siasa Mkoa na Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Mkoa.
Amesema kuwa inasikitisha kuona
Vijana wa UVCCM Mkoa wa Pwani, wanatoa matamko kuwa Rais ajaye 2015
hatatoka kanda ya Kaskazini na anayemfahamu ni Rais peke yake ambaye ni
Jakaya Kikwete.
Millya alisema cha kusikitisha
pale alipokemea kauli hiyo alipuuzwa na hadi sasa Ikulu haijawahi kutoa
kemeo kwa Vijana hao na wala kukataza kauli hizo kutolewa, jambo
lililompa jibu kuwa Ikulu inahusika kwa namna moja au nyingine na kauli
hiyo.
Aidha alisema kuna Vijana wengi
walioko ndani ya CCM wakiishi kwa matumaini ya kusubiri kuteuliwa
nafasi ya Mkuu wa Wilaya kama sio Mkoa, ila yeye hawezi kuishi kw
amatumaini kama muathirika wa Ukimwi.
Hata hivyo alitoa wito kwa
Vijana wote wenye nia ya dhati na mapenzi mema ya nchi yao, kumfuata
Chadema ambako kunatoa tumaini jipya la maisha ya watu.
Comments