Skip to main content

WANAHARAKATI WATAKA MJADALA KUHUSU ULEVI UNAVYOCHANGIA UKATILI


 Ananilea Nkya Mkurugenzi Mtendaji Tamwa
---
 
Viongozi wa mashiriki matatu  yanayotetea  haki za wanawake na watoto wamesema ni muhimu  wananchi mijini na vijijini wakaanza kujadili madhara ya ulevi na kuchukua hatua  kuepusha  vitendo vya ukatili vinavyosababishwa na ulevi.

 Wamesema bila jamii kuchukua hatua madhubuti kupambana na ulevi nchi itaendelea kushuhudia vitendo vya ukatili wa kijinsia  vinavyokosesha familia  amani  ambayo ni msingi  muhimu wa maendeleo ya familia na taifa.

Wamesema wanaume wanaokunywa pombe na kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wanaweza kubadilika endapo wananchi  katika ngazi za  vijiji, mitaa na kwenye  taasisi wangeanzisha mjadala kuhusu namna bora ya kupambana na ulevi.

 Viongozi hao  kutoka  Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Shirika la Haki za  Wanawake – KIVULINI na  Kituo cha Usuluishi (CRC) walisema hayo walipokuwa wakizungumza na TAMWA kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki.

 Wamesema  kwa mfano matukio mengi ya wanawaume kuwapiga wake zao, ubakaji, lugha za  kudhalilisha utu,  na wazazi kutohudumia watoto kwa kuwapatia  chakula, mavazi  na elimu  yanachangiwa na ulevi.

 Maimuna Kanyamala, Mkurugenzi wa  shirika la KIVULINI ambalo linaendesha kampeni ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake katika kanda ya Ziwa  amesema kupitia sinema na mijadala ya umma wanaume zaidi ya 350,000 katika kanda hiyo wamebadilika  na familia zao zinaishi kwa amani.

 Amesema watu hao waliweza kuacha pombe baada ya kuona sinema iliyoonyesha mambo maovu ambayo mtu anaweza kufanya kutokana na kunywa pombe.

 Mkurugenzi wa WLAC  Theodosia Muhulo Nshala na  Mratibu wa CRC  Elizabeth  Muhangwa wamesema  wanawake wengi   na watoto wanaofika katika mashirika  yao kutaka msaada wa ushauri na wa kisheria   ni wale ambao wamefanyiwa ukatili ambao kwa namna moja au nyingine umechochewa na  unywaji wa pombe. Viongozi wa mashirika hayo wameyataka mashirika yote ya kijamii yanayotoa msaada wa kisheria na ushauri kwa wanawake na watoto kuchunguza kwa kina mashauri wanayopokea ili kufahamu ni yepi yana uhusiano na pombe.
 
 Wamesema kwa kufanya hivyo nchi itaweza kupata takwimu sahihi kuhusu ni kwa kiasi gani unywaji pombe unavyochangia ukubwa wa tatizo la ukatili wa kijinsia.


                                                Imetolewa na: 
Ananilea Nkya
Mkurugenzi Mtendaji Tamwa

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...