Mbunge
wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe akisaini karatasi inayokusanya saini
za wabunge za kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa lengo la kuwasilisha
kwa Spika mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni,
Kabwe Zitto.
UKUSANYAJI saini za wabunge kwa ajili ya kuwasilisha azimio la kutokuwa na imani na Waziri Mkuu umechangamkiwa lakini kuna mgawanyiko baina ya wabunge wa CCM kwa kuwa baadhi yao wanapinga azimio hilo.
Hadi jana saa 9 alasiri, wabunge watano wa CCM ndiyo walikuwa wamesaini akiwemo Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, aliyesaini akikanusha kutumwa na mtu kwa kusema hana haja na uwaziri, kama ambavyo baadhi ya wabunge walivyowatuhumu kuwa wanaoshinikiza azimio hilo wanataka uwaziri.
Wanaoponda hoja hiyo wanasema haina mashiko, kwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hahusiki na uteuzi wa mawaziri.
Mbunge aliyezungumza hadharani na waandishi akipinga, ni wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM) ambaye amemtetea Pinda kwamba ni mtendaji mzuri na hajavunja maadili yoyote kiasi cha kuruhusu hoja ya kumwondoa kuwa na mashiko.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema) ndiye aliyeongoza kazi hiyo jana na hadi saa 9, zilishakusanywa saini 66 za wabunge kutoka vyama vyote isipokuwa United Democratic Party (UDP) ambacho mbunge wake ni John Cheyo ambaye pia ni Mwenyekiti.
Akiongozana na Filikunjombe, Zitto aliwaambia waandishi wa habari kwamba hadi muda huo, idadi ya wabunge wa CCM waliosaini ni watano, CUF 12 na wengine ni waTLP, NCCR-Mageuzi na Chadema.Inatoka kwa Mdau.

Comments