Kwaya ijulikanayo kama Kwaya ya
Ng'ombe ya Magu Mjini Mkoani Mwanza yenye watu 45 imejiengua CCM na
kuhamia CHADEMA. Wanakwaya hao wamepokelewa na Mwenyekiti wa CHADEMA
Wilaya ya Magu ndugu Katinde aliyeongozana na Katibu wa CHADEMA Jimbo
la Magu mjini Bahati Simon.
Hii ilikuwa ni Kwaya ya waliyoitumia sana kwenye kampeni na kwenye kila matukio yao na vifaa vyao vyote vya muziki vilitunzwa kwenye ofisi za CCM wilaya ya Magu. Siku mbili kabla ya kuhamia CHADEMA walitafuta kambi ya muda na wakatunga nyimbo za kumsifia Dr. Slaa ambaye atafanya ziara hivi karibuni wilayani Magu.Inatoka kwa Mdau.

Comments