Maji
bado ni tatizo hususani katika Mkoa wa Dodoma ambapo wakazi wengi wa
Mkoani Dodoma hususani maeneo ya vijijini hupata maji ambayo siyo safi
na salama kama ambavyo kijana huyu ambaye hakupenda jina lake kuchorwa
mtandaoni alipokutwa na Mtandao wa Lukaza Blog akiwa ametoka kuchota
maji kwaajili ya matumizi ya nyumbani kwao maji yenyewe ndo ayo kama
yanavyoonekana. Kijana Huyu anaishi Maeneo ya Ntyuka Mbali kidogo na
Dodoma Mjini ndani ya Manispaa ya Dodoma.
Akiongea
na Mtandao wa LUKAZA blog, kijana huyu alisema kuwa achilia mbali
umbali wanaokwenda kuchota maji bali hata maji wanayoyapata sio safi na
salama katika matumizi ya binadamu lakini kwasababu ni Shida basi
hawana budi Kuchota na kutumia japokuwa wanajua kuwa maji hayo ambayo
sio safi na salama huweza kuleta magonjwa lakini huwa wanamuachia Mungu
Kwa Kulinda Maisha Yao.
Aliongezea
Kwa Kusema Kuwa tokea azaliwe hajawahi kuona maji ya bomba yanafananaje
na kusema kuwa ameshazoea maji hayo na hayajawahi kumletea madhara
yoyote yale
Picha NaShax Ngeta Wa Lukaza Blog.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments