SMZ haitakivumilia Kikundi chochote kitakachoonekana kuhatarisha Amani, Utulivu na Umoja wa Visiwa hivi vya Unguja na Pemba.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi wakati akifunga Mkutano wa Saba wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar huko Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif alitahadharisha kwamba Serikali haitasita kukizuia Kikundi
chochote kinachoendesha mihadhara au Makongamano yatakayobainika
yanahatarisha usalama wa Nchi.
Alisema Serikali haikatazi Kuendeshwa kwa mihadhara na Makongamano na ndio maana ikavumilia ikidhani kuwa nia ya mihadhara hiyo ni kuelimisha Jamii. Alisema hivi karibuni kipo kikundi kinachoendesha Mihadhara na Makongamano inayotishia hali ya Amani na Utulivu kwa kuhamasisha kwa nguvu watu kuukataa Muungano huku wakitukana kwa nguvu zote Viongozi wa Taifa hili wakiwemo wanaounga Muungano.
“Mihadhara hiyo imebadilika sura na badala ya kuelimisha imekuwa ni uwanja wa kashfa, kejeli na matusi ya nguoni kwa Viongozi wetu, jambo ambalo ni kinyume kabisa na utamaduni wa Mzanzibari na Misingi ya Kidemokrasia. Kwa hili hatutokuwa na muhali a Mtu wals Kikundi chochote” Alikemea Balozi Seif. Balozi Seif aliwaomba Wananchi kuwa fursa iliyotolewa na Serikali zote mbili kwa kuleta mchakato wa Katiba mpya ni jambo la Kihistoria na linaonyesha kukua kwa Demokrasia Nchini Tanzania.
Akizungumzia uimarishaji wa Zao la Karafuu Serikali imejiandaa kuhakikisha miche ya Mikarafuu inapatikana katika Vitalu vyake vyote na kwamba wakulima wote Nchini watapatiwa Miche hiyo bila ya malipo.

Comments