Francois
Hollande kutoka chama cha Kisoshalisti nchini Ufaransa ambaye anataka
kuwahudumia vizuri zaidi watu masikini na wale wasiokuwa na ajira
anaiingia duru ya pili ya uchaguzi wa rais dhidi ya Rais Nicolas
Sarkozy.
Uchaguzi huu unaweza kubadili ramani ya kisiasa na kiuchumi barani Ulaya.Katika uchaguzi huo uliofanyika Jumapili (22.04.2012) nchini Ufaransa hakuweza kupatikana mshindi wa moja kwa moja na hiyo kulazimika kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi hapo tarehe 6 Mei.
Huyo ni Francois Hollande ambaye anaingia duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Ufaransa akiwa anaongoza katika kura kwa kumpita chupuchupu mhafidhina Sarkozy alienadi kampeni yake kwa kutumia ilani ya kudhibiti uhamiaji katika dura ya kwanza ya uchaguzi huo.
Mshangao mkubwa kabisa wa uchaguzi huo ni kwamba katika kila wapiga kura watano mmoja amemchaguwa mgombea wa sera kali za mrengo wa kulia Marine Le Pen na kumfanya ashike nafasi ya tatu na pia nafasi ya kuwa na usemi katika siasa za Ufaransa kwa kutumia ilani ya kupinga uhamiaji ambayo inawalenga mamilioni ya Waislamu wa Ufaransa.
Ikiwa asilimia 93 ya kura zikiwa tayari zimekwishahesabiwa Hollande amejipatia asilimia 28.4 ya kura,Sarkozy amejipatia asilimia 27 na Le Pen ambaye ameshika nafasi ya tatu amejipatia asilimia 18.3 ya kura ,ambayo ni matokeo mazuri kabisa kuwahi kushuhudiwa na chama cha National Front kilichoasisiwa na baba yake Jean- Marie Le Pen. Idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ni kubwa ambapo imepindukia asilimia 80 katika uchaguzi huo wa urais uliokuwa na wagombea 10.

Comments