Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw. Ephraim
Mafuru akitangaza rasmi mbele ya waandishi wa habari promosheni kabambe
ya vinywaji vya kampuni hiyo inayoitwa Vumbua Hazina chini ya Kizibo,
ambapo zaidi ya shilingi milioni 700 zitashindaniwa zikiwemo fedha,
pikipiki, Bajaji na Magari manne.
Bia zitakazohusika katika promosheni hiyo ni Pilsner Ice, Tusker
Lager na Serengeti Lager na watu watashiriki promosheni hiyo kupitia kwa
kutuma ujumbe wa namba zilizopo katika vizibo vya bia hizo kupitia
mitandao mbalimbali na kupokea zawadi zao kupitia M-Pesa baada ya
kushinda. Promosheni hiyo inaanza jumanne Aprili 24.
Katika picha kulia ni Mtaalam wa Bidhaa SBL Bw. Maurice Njowoka na
kushoto ni Asia Natalia MhinaMkuzaji wa Biashara ya M-Pesa kutoka
Vodacom Tanzania.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti SBL Bw. Ephraim
Mafuru akielekeza zawadi zitakazoshindaniwa katika promosheni hiyo kulia
ni Asia Natalia MhinaMkuzaji wa Biashara ya M-Pesa kutoka Vodacom
Tanzania na katikati ni Mtaalam wa Bidhaa SBL Bw. Maurice Njowoka.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
Wadau ktoka kampuni ya Push Mobile wakiwa katika mkutano huo.
Wadau kutoka kampuni ya R&R wakipozi kwa picha.
Wadau kutoka kampuni ya bia ya SBL wakiwa katika picha ya pamoja.
Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kupitia vinywaji vyake bora
kabisa vya Serengeti premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager iameandaa
promosheni kubwa na ya aina yake itakayofanyika Tanzania nzima katika
kipindi cha wiki 16 ambapo zawadi mbalimbali zitashindaniwa.
Promosheni hiyo ya aina yake imesheheni zawadi mbalimbali kubwa na
ndogo kama vile Jenereta 16 , Pikipiki 8, Bajaji 8, Gari ndogo maarufu
kama saloon car 8, pamoja na zawadi zingine nyingi ambapo kila baada
ya wiki mbili gari 1 aina ya saloon itakuwa inashindaniwa, kila
baada ya wiki mbili Bajaji 1 itakuwa inashindaniwa, kila baada ya wiki
Pikipiki moja itashindaniwa na kila baada ya wiki moja Jenereta moja
itakuwa inashindaniwa.
Akizungumzia promosheni hiyo kabambe Mkurugenzi wa masoko wa
kampuni ya bia ya Serengeti, bwana Ephraim Mafuru amesema promosheni
hiyo sio tu inalenga kuongeza mauzo ya vinywaji hivyo bali pia inalenga
kuinua na kubadilisha maisha ya watanzania hususani wateja wa bidhaa
zinazozalishwa na kampuni hiyo ikiwa ni sera mojawapo ya kampuni hiyo
kuisaidia jamii kwa njia mbalimbali kupitia bidhaa zake zenye ubora
wa aina yake.
“Kampuni yetu imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo
ya taifa letu katika maeneo mbalimbli kupitia jamii inayotuzunguka na
wateja wetu kimaisha, hivyo promosheni hii pamoja na ukweli kuwa inalenga
kuongeza tija katika masoko ya bidhaa zetu bado unaweza kuona zawadi
zitakazoshindaniwa katika promosheni hii ni zawadi kubwa ambazo kwa
namna moja ama nyingine inaweza kubadilisha maisha ya mshindi wetu kutoka
hatua aliokuwepo hadi hatua nyingine, kwa hivyo sisi SBL tunasema tunajivunia
kuwa sehemu mojawapo inayochangia maendeleo ya watanzania wateja wetu
na taifa kwa ujumla” alisema bwana Mafuru.
Kwa upande wake Meneja wa bia ya Tusker Lager, Bi Rita Mchaki, amesema
kampuni ya bia ya Serengeti inazalisha bidhaa zinazopendwa na watanzania
wengi kutokana na ubora wa kipekee wa bidhaa hiyo, na kwamba promosheni
hiyo kabambe nisawa nakurudisha shukrani zake kwa watanzania kwa kufanikisha
kampuni hiyo kufikia malengo yake kibiashara.
Watanzania wote wenye umri wa miaka 18 na zaidi na wanaotumia bidhaa
zetu zilizoainishwa katika promosheni hii wanaombwa kushiriki kwa wingi
bila kukata tamaa kwani zawadi zinazoshindaniwa zinaweza kubadilisha
maisha kwa yeyote atakayebahatika kuibuka na ushindi.Inatoka kwa Lukaza.
Comments