Uamuzi ambao wameutoa
Africa Magic Swahili baada kifo cha Steven Kanumba ni kwamba mwezi huu
wote wa April wameamua kuuita MWEZI WA STEVEN KANUMBA ambapo
wataonyesha movie zote za Kanumba kwa kipindi hicho.Africa Magic
Swahili ni channel inayopatikana kwenye DSTV, Channel ambayo ni maalum
kwa ajili ya kuonyesha movie za Kiswahili.
Afisa uhusiano wa
Multichoice Tanzania Barbara Kambogi amesema “Africa Magic wamefanya
kazi kwa ukaribu sana na Kanumba, hata Africa Magic Swahili
ilivyozinduliwa hapa Tanzania mwaka jana Kanumba alikua mmoja wa
wasanii walioisupport sana, ni channel ambayo inatoa nafasi ya wasanii
wa Tanzania kuweza kuuza movie zao na kuonekana Africa nzima” “Kanumba
alikua asafiri Alhamisi kwenda Marekani kwa ajili ya kupromote movie
yake mpya ambayo aliizindua na nasikia hiyo movie inafanya vizuri sana
Ghana, tunatarajia kwamba kila kitu kikishakamilika baadae pia hiyo
movie itarushwa kwenye channel ya Africa Magic Swahili”
Comments