NEW YORK,Marekani
MUIGIZAJI Angelina Jolie na Brad Pitt wamethibitisha kuwa wanajiandaa kufunga pingu za maisha
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mwishoni mwa wiki wapendanao hao tayari wameshavalishana pete ya uchumba ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ndoa hiyo.
Ndiyo wameshathibitisha ,Meneja wa Pitt, Cynthia Pett-Dante aliliambia jarida la Watu . Wameshatoa ahadi ya kuishi pamoja na watoto wao wanafurahi lakini hakuna tarehe ambayo imeshapangwa,"aliongeza meneja huyo.
Meneja huyo alisema kwamba sonara Robert Procop ndiye aliyemtengenezea pete ya uchumba Jolie kwa kushirikiana na Pitt.
Ndiyo naweza kuthibitisha kwamba Robert Procop ndiye aliyebuni pete ya uchumba ya Angelina Jolie, kwa kushirikiana na Brad Pitt, alisema msemaji wa Robert.

Comments