Takriban
watu watatu wameuawa katika shambulio lililotokea kwenye ofisi za
kampuni moja ya kuchapisha magazeti katika mji mkuu Abuja,Nigeria
wafanyakazi wa huduma za dharura wanasema.
Kuna taarifa pia za vifo vya watu wengine watatu baada ya shambulio lingine la bomu katika mji wa kaskazini wa Kaduna kutokea.
Shambulio
la mjini Abuja katika kampuni ya gazeti la ThisDay lilitokana na bomu,
msemaji wa halmashauri ya shughuli za dharura za kitaifa amesema.

Comments