Na
nyie kina kaka punguzeni kuchagua, kwa mfano huoni kuwa ni risk kuanza
kutaka kufanya mapenzi na msichana mapema hii na kwa yule aliyesema
kuwa wengine wanakubali kirahisi, sasa kwa nini umuombe tendo la ndoa?
Kwanini
usifanye urafiki wa kawaida kwanza bila kufanya mapenzi, mkazoeana
mkajuana tabia kama ni wa dizaini ya kutaka mali au wa kujenga, kisha
ndio mkaenda stage nyingine? Hivi ngoja leo niwape dillema
mnayowatwisha kina dada.
Kwa
mfano dada wa watu keshakaa wee miaka hatokei mtu wa kumuomba uchumba,
mara leo hii umetokea wewe unamtaka urafiki na mara unatanguliza kuomba
ngono, hapo anakuwa kwenye dillema, akikukatalia utaingia mitini kimoja
na yeye kubaki mpweke. Sasa akupe ngono au abaki mpweke? Na pengine
huko nyuma alishakutana na kina kaka maguberi yakataka ngono akakataa
ana kaachwa solemba! Sasa hapo afanyeje akukubali umtose vile vile kwa
kumuona yu rahisi au akukatalie a risk loneliness!
Kisha swali la kizushi, kama mtu umempenda kwa nini umtie hiyo mitihani ya kuanza kumuomba ngono? Ndio kujionyesha Urijali au? Na kwa kuwa umeomba mwenyewe kwa nini ukipewa uanze kuwa na mashaka kama si unafiki ni nini? Sasa ulikuwa unaomba ili ukataliwe? Na msichana akikukubalia haina maana kuwa ni mrahisi bali pengine amekuzimia muda ila ameshindwa kukwambia anasubiri golden chance na hiyo umeileta sasa afanyaje?
Cha msingi ni kuwa muwazi na mkweli. Mweleze wazi mwenzako, kusiwe na unafiki, kama kuna mpango wa kuoana basi na muwe marafiki kama ni mpango wa kuchezeana basi na mwambie aanze mbele ili asikuzibie wengine wakafikiri una mtu kumbe huna kitu! Lakini pia ukiwa bold wanaume wengine wanashangaa wanataka wao ndio waanze kutangaza ndoa!

Comments