Skip to main content

TGNP YALIA NA MAWAZIRI NA WATENDAJI WASIO WAJIBIKA




MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) imeitaka Serikali kuwawajibisha mara moja mawaziri, manaibu waziri na watendaji wakuu wa Serikali na mashirika ya umma ambao wametajwa kuhusika na matumizi mabaya ya fedha za umma ama kushindwa kusimamia rasilimali za taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Anna Kikwa katika taarifa yake aliyoisambaza kwa vyombo vya habari. Aidha amemtaka mkuu wa nchi awafute kazi watendaji wanaotumia vibaya fedha za umma na kuwaongezea wananchi umasikini, ili iwe fundisho kwa watendaji wa Serikali wenye tabia kama hiyo na wachukuliwe hatua za kisheria.

Hata hivyo TGNP imeishauri Serikali kuboresha mifumo ya kusimamia rasilimali za nchi yetu ili wananchi wote waweze kufaidi keki ya taifa kwa sababu mara zote Serikali imekuwa ikisema Tanzania hatuna rasilimali lakini hali halisi ni kwamba rasilimali za taifa zinaliwa na mafisadi wachache wa ndani na nje ya nchi.
Katika hatua nyingine, mtandao huo umetoa pongezi kwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu, Ardhi Maliasili na Utalii kwa kusimamia vema na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali zinazotokana na walipa kodi na kuwasilisha ripoti zao Bungeni ambazo zimeibua uozo mkubwa na kujenga mjadala mpana unaotaka uwajibikaji kwa wanaohusika.
“Tunawapongeza pia baadhi ya wabunge walioshiriki katika mijadala kwa kuzijadili ripoti hizo kwa undani bila kujali urafiki, itikadi za kisiasa, hasa ile ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kuibua uozo uliojificha na kusimamia maslahi ya Taifa.” amesema Bi. Kikwa katika taarifa hiyo.
“Tumeshuhudia mara kadhaa kupitia vyombo vya habari wabunge wakiacha itikadi zao za kisiasa na kusimamia kwa dhati dhana ya kushinikiza uwajibikaji katika vyombo vinavyohusika kutokana na ufisadi kama Richmond, Dowans nk. Hata hivyo, TGNP kwa muda mrefu tumekuwa tukipinga ubadhirifu wa fedha za umma na kudai haki ili kutokomeza ufisadi uliokithiri, lakini bado ufisadi umezidi kushamiri hasa katika Wizara na taasisi za umma.
“Sisi kama wanaharakati tunasema kuendelea kwa ufisadi ni aibu kwa serikali iliyoko madarakani, TGNP tuko mstari wa mbele kushinikiza rasilimali za taifa ziwanufaishe wananchi wote, hasa walioko pembezoni, kamwe hatutanyamazia aina yoyote ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za miradi ya wananchi zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.” Imesema taarifa hiyo.
"Tumeshuhudia wanawake na wasichana wakiendelea kuwa maskini na kukumbana na mifumo kandamizi kwa kukosa haki za kufikia huduma za msingi kama vile maji, barabara, afya, elimu, kilimo, utawala bora n.k. Fedha zinazopotea zinatokana na kodi za wananchi na jamii ina haki ya kuhoji uwajibikaji na wahusika wanatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria," imeongeza taarifa hiyo kwa vyombo vya habari.
Vilevile tunawapongeza wabunge wote walioshiriki kwa dhati katika zoezi la kusaini kusudio la kutaka viongozi waliotajwa/kutuhumiwa kwenye ripoti hizo kuwajibika. Ili kuonesha dhana ya uwajibikaji na utawala bora unaozingatia misingi ya haki za binadamu.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was

HAYA NI MAKAO MAKUU YA MTANDAO WA Tigo TANZANIA DAR ES SALAAM

MAHALA yalipo ni Lugoda Street Gerezani Industrial Area , kwa sasa mdandao huu umefanya makubwa , kuna Tigo Bwerere Uilisha cheki hiyoooooo watu full kujiachia wana chonga tuu kwenye vyao vilonga.