NA GAZETI LA MWANANCHI: WABUNGE 73 WASAINI,SPIKA ATUMIA KANUNI KUUZIMA,ZITTO ASEMA WANAWEWESEKA ZOEZI LINAENDELEA
Mbunge wa Ludewa
(CCM), Deo Filikunjombe akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge
wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika Viwanja vya
Bunge mjini Dodoma jana.
Kulia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anayefanya zoezi la kukusanya sahihi za wabunge ili aweze kuwasilisha bungeni hoja kutokuwa na imani na waziri mkuu. Picha na Edwin Mjwahuzi
Mkakati wa kukusanya majina 70 ya wabunge kama sehemu ya kukamilisha utaratibu wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, umepamba moto na hadi kufikia jana jioni, wabunge 75 walikuwa wameunga mkono hatua hiyo, watano kati yao, wakitokea chama tawala CCM.
Kwa mujibu wa Mwananchi endapo mchakato huo utakamilika, Pinda atakuwa ameingia katika historia ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na Bunge, tangu Tanzania ipate uhuru wake Desemba 9, 1961.
Hata hivyo wakati mchakato huo ukiendelea, Spika wa Bunge, Anne Makinda jana jioni aliibuka bungeni na kueleza kuwa mchakato huo ni batili.Kusoma zaidi bofya
Akinukuu vifungu vya Kanuni za Bunge na Katiba, Spika Makinda alisema mkakati huo ni batili kwa kuwa kanuni zinaeleza bayana kuwa ulipaswa kufanyika siku 14 kabla ya kuwasilisha hoja hiyo kwa Spika.
“Bunge letu linaisha Jumatatu ambayo ni siku nne tu tangu leo (jana) na kwa mujibu wa kanuni, taarifa ya maandishi iliyotiwa saini na kuungwa na wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote, itatolewa kwa Spika siku angalau 14 kabla ya siku inapokusudiwa kuwasilishwa bungeni.”
Spika Makinda alisema pamoja na hayo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe aliyeongoza mchakato wa kukusanya saini hizo za wabunge, alikuwa sahihi kuendesha mpango huo kwa mujibu wa Kanuni ya 133 ya Bunge na Ibara ya 53 (3)ya Katiba.

Comments