Washiriki
wa kitongoji Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012, wakiwa
katika picha ya pamoja,tayari kuchuana vikali Mei 5 2012 ndani ya
hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la
Arusha.katika shindano hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni kwa viti maalum
ni sh.25,000/= na kwa viti vya kawaida ni sh 15,000/=
Washiriki
wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa darasani kwenye mafunzo ya
nadharia yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving
School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo.
Washiriki
wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo
yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia
ni moja ya wadhamini wa shindano hilo
Mashindano
ya Ulimbwende ngazi ya kitongoji Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City
Center 2012,yanatarajiwa kufanyika Mei 5 2012 ndani ya hoteli ya
Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.
Akizungumza
leo jijini Arusha,Mratibu wa shindano hilo Bi Upendo Simwita kutoka
kampuni ya Tour Visual Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano
hilo,amebainisha kuwa mpaka sasa maandalizi yao yanakwenda vizuri na
kila kitu kimekwisha kamililka ikiwemo sambamba na kuwapata warembo
ambao mpaka sasa wametimia 20.
Bi
Upendo Simwita amesema kuwa wameishakamilisha mchakato wa kuwapata
Warembo wenye mvuto na wenye vigezo stahiki,anaongeza kuwa warembo hao
wenye ari kubwa ya ushindani,kama waandaji watahakikisha muwakilishi wa
Miss Tanzania 2012 anatokea kwenye kitongoji hicho.
“Shindano
hilo litakalokuwa la tofauti kubwa na miaka ya nyuma litawakutanisha
walimbwende wapatao 20,ambao watachuana vikali jukwaani, na hatimaye
kumpata Mshindi wa Miss Arusha City Center”,alisema Upendo.Amesema kuwa
kiingilia katika shindano hilo kimepangwa kuwa ni kwa viti Maalum sh
25,000/= na kwa viti vya kawaida sh.15,000/=. Fanya booking yako ya
tiketi mapema kupitia namba – 0755975454 au 0713681059.
Kwa
upande wa Burudani,Upendo amesema kuwa kutakuwepo na Msanii mahiri wa
Muziki wa kizazi kipya aitwaye Sam wa Ukweli,Muziki wa Asili,Live Band
ya Watoto wa Simba pamoja na burudani nyingine mbalimbali
zitakazotolewa na walimbwende wenyewe siku hiyo.
Upendo
amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni REDD’S ORIGINAL,NAURA
SPRINGS HOTEL,CLAUDS FM / CLAUDS TV AND MAWINGU CLUB – ARUSHA,BG
HORIZON, MODERN DRIVING SCHOOL,MAKO ADVENTURE,SEBE & BEKI FOR LIFE, MWANDAGO
INVESTMENT,S.G. RESORT,MEJA LINK LTD,GEO SECURITY,GOLDEN ROSE
HOTEL,RIVERSIDE SHUTTLE SERVICES,ARUSHA TRAVEL LODGE,LITTLE ROSES, LA BELLA VISTA,WAKIPAMBWA NA JANETH BEAUTY.Inatoka kwa LUkaza.
Comments