Na Elisante John
Singida
MAHAKAMA
kuu kanda ya Dodoma imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na wanachama
wawili wa CCM, kupinga ushindi uliompa ubunge wa Jimbo la Singida,Tundu
Lissu (CHADEMA).
Akisoma
hukumu hiyo, iliyochukua saa nne, Jaji Moses Mzuna wa Moshi, mkoani
Kilimanjaro, alisema wadai wameshindwa kuthibitisha hoja 11
walizomtuhumu Lissu, msimamizi wa uchaguzi na mwanasheria wa Serikali.
Alisema,
baada ya mashahidi 24 wa upande wa wadai kutoa ushahidi wao na wanne wa
wadaiwa, ameona uchaguzi huo ulikuwa huru, haki na ulifuata taratibu
zote, hivyo hauhitaji kutenguliwa.
Baada
ya hukumu na Jaji kutoka mahakamani ,Lissu alishindwa kujizuia na
alianza kulia huku akitoa machozi ya furah na kuwapa wakati mgumu,jamaa
na wafuasi wa CHADEMA, kumbembeleza.
Baadhi
ya wabunge wa CHADEMA waliokuwepo mahakamani kusikiliza hukumu hiyo ni
Israel Natse-Karatu, Paulina Gekul na Rose Kamili wa viti maalumu,
mkoa wa Manyara.
Wengine ni Christina Mughwai na Christowaja Mtinda, wote viti maalumu, mkoa Singida.
Kesi
hiyo ilisikilizwa mfululizo kuanzia Machi 12, 2012, walalamikaji ni
Shabani Selema Itambu na Pascal Masele Hallu, wakazi wa kijiji cha
Mkiungu, Singida vijijini.
Wadai
walitetewa na wakili Godfrey Wasonga, wa kampuni ya Wasonga $
Associates Advocates ya Dodoma, wakati Lissu alisimamia mwenyewe,
akishirikiana na wanasheria watatu wa serikali, Vicent Tangoh, Juma
Ramadhani na Abdallah Chavula.
“Matakwa
ya wananchi yaweza kuheshimiwa….kupepeta tu mdomo, bila ya kuwa na
ushahidi wa kuthibitisha, ukitengua matokeo hivi hivi tu, wengi
utawaharibia, siyo tu uchaguzi, bali hata maisha yao ya
baadaye,’alisema Jaji Mzuna.
Baada
ya kutoka nje ya mahakama, Lissu aliishukuru mahakama na kwa maamuzi
sahihi hadi kushinda kesi hiyo,huku akisema haki ya mtu haipotei.
Aliondoka
viwanja vya mahakama akisindikizwa na magari ya polisi, wakiongozwa na
OCD wilaya, msululu wa magari ya wafuasi wa CHADEMA, waliojawa
na furaha kuu tele, waki wilaya mpya ya Ikungi, kwa mkutano hadhara.
Naye mmoja
wa wadai wa kesi hiyo, Shabani Itambu, alisema kwa kuwa kesi hiyo ni ya
chama chake (CCM), atakutana na viongozi wake na wakili, wajue cha
kufanya.Inatoka kwa Mjengwa.
Comments