Mwigizaji Ruth Suka
‘Mainda’ amesema kuwa baada ya filamu zake kadhaa kuingia sokoni na
kufanya vizuri anatarajia kuingiza filamu mpya sokoni inayokwenda kwa
jina la Mke mwema ambayo amefanikiwa kuirekodi hivi karibuni na
kushirikisha wasanii wakali katika tasnia ya filamu hapa nchini. “Kwa
mwaka huu nimepanga uwe wa kazi kwa kwenda mbele nimemalizia filamu
mpya kabisa na ya kusisimua ya Mke mwema ambayo natarajia kuiingiza
sokoni wakati wowote kuanzia sasa kwani kila kitu kipo poa ndio maana
naweza kufanya chochote kwa ajili ya filamu hii,”anasema Mainda. Filamu
hiyo ambayo imeigizwa katika mazingira ya kijamii tena maisha ya
Kijijini inaonyesha jinsi gani mke anavyoweza kujenga nyumba katika
familia kama alivyofanya Mainda kwa kumrudisha mumewe na kuijali
familia, filamu ya Mke mwema imeshirikisha wasanii kama Jengua, Steve
Nyerere ambaye ni mumewe, Mainda mwenyewe, John Mafufu pamoja na
wasanii wengine.
Chanzo ni Pro24.
Chanzo ni Pro24.
Comments