Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameoa mke wa nne, kwenye sherehe ya kijadi ambapo wake zake wengine watatu pia walihudhuria.
Bwana
Zuma, mwenye umri wa miaka 70, alivalia ngozi ya chui na kubeba mkuki
na ngao, mavazi ya jadi ya Kizulu, kwenye harusi iliyofanywa jimbo la
KwaZulu-Natal.
Wakuu wanasisitiza kuwa Bwana Zuma mwenyewe anagharamia sherehe hizo za wikiendi hii.
Bi harusi Bongi Ngema, amefuatana na Rais Zuma kwenye ziara zake rasmi kwa miaka kadha.
Bi harusi Bongi Ngema, amefuatana na Rais Zuma kwenye ziara zake rasmi kwa miaka kadha.
Comments