Mwanafunzi
wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Alfa Morogoro, Jesca
Kiliani (17) akifanya mtihani wa taifa wa kidato hicho akiwa wadi namba
7B katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo jana, baada ya kulazwa
kufuatia kufanyiwa operesheni ya uvimbe ambapo hivi sasa anaendelea na
matibabu hospitalini hapo.Inatoka kwa mdau.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu


Comments