Na Khaleed Gwiji Zanzibar
Viongozi wa Uamsho wamepelekwa rumande baada ya Hakimu wa Mahakama ya
Wilaya iliyopo Mwanakwerekwe, Zanzibar, kuwanyima haki yao ya dhamana.
Ulinzi katika Mahakama hiyo na maeneo yaliyo pembezoni mwake ulikuwa ni mkali mno asubuhi ya leohadi kumaliza kwa shauri husika.
Washtakiwa walipandishwa kizimbani mnamo majira ya saa tano akiwemo: Sh.
Mselem, Sh. Farid, Sh. Azzan, Sh. Mussa, Sh. Suleiman, Sh. Khamis na
Nd. Hassan. Wote walisomewa shtaka lao baada ya kusomwa Hati ya Mashtaka
(Charge Sheet) na Wakili wa Serikali anaetoka Afisi ya Mkurugenzi wa
Mashtaka, Zanzibar ambayo pamoja na maelezo mengine, inaeleza shtaka
hilo kuwa ni: matamko ya uchochezi yaliyopelekea kufanyika kwa fujo na
uvunjifu wa amani yaliyotolewa tarehe 17, August, 2012, Magogoni,
Zanzibar.
Baada ya washtakiwa kusomewa shtaka na wote kulikataa, Wakili wa
Serikali aliiomba Mahakama kuipangia kesi tarehe nyengine kwa kuwa
upelelezi hakuwa umekamilika.
Unade wa Mawakili wa washtakiwa ukiongozwa na Mh. Abdallah Juma na
wenziwe wawili: Mh. Rajab na Mh. Suleiman kwa pamoja waliiomba Mahakama
mambo mawili:
Moja, wapatiwe Hati ya Mashtaka (Charge Sheet) ili kupitia kwayo wataweza kuwatetea wateja wao kwa ubora zaidi.
Pili, waliiomba Mahakama kuwapatia washtakiwa wote 7 dhamana zao sio tu
kwa kuzingatia kwamba dhamana ni haki ya washtakiwa ya Kikatiba; bali
pia kutokana na nature ya shtaka lenyewe la incitement to violence
ambalo ni kosa dogo (misdemeanour) na hivyo kulifanya kuwa ni bialable
offence.
Comments