Wakati
Zanzibar Sakata la Waislamu kuendeleza kitimtim kufuatia kutoonekana
kwa Kiongozi wa Kundi la Uamsho Vurugu zimeendelea kutawala eneo la
Darajani na kusababisha Polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi
kutawanya watu.
Jijini Dar es Salaam hali si tofauti na hiyo maeneo ya Kariakoo maduka
kadhaa yamefungwa kufuatia vurugu kama hizo baada ya Swala ya Ijumaa
kufuatia pia kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Tanzania Sheikh Ponda yamekuwa ni matokeo ya vurugu watu kukimbizana
huku Polisi wakidhibiti Usalama na Amani kuelekea harijojo.(Picha na
Maktaba).
Maeneo ya Posta karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani Askari wameweka utepe
wa kudhibiti watu kuingia katika maeneo hayo kitendo kilichosababisha
shughuli nyingi kusimama.
Pichani
ni Jeshi la Wananchi Tanzania likiwasilia maeneo ya Kariakoo kuongezea
nguvu kwa ajili ya kutuliza ghasia. (Picha hii imepigwa na mdau Mpeli Jr
Ngonywike kupitia mtandao wa facebook alipopiga picha hii kwa
kujificha.
Comments